Friday, 25 July 2014

NYOTA WAPYA WALIOTUA LIVERPOOL WAMTOA JASHO RAHEEM STERLING


We go again! Raheem Sterling knows he has to prove himself all over again
Tumelianzisha tena! Raheem Sterling anajua wazi kuwa anatakiwa kujithibitsha mwenyewe kuwa ni bora.

 

LICHA ya kuwa miongoni mwa wachezaji wachache wa England waliorudi na heshima kutoka kombe la dunia, Raheem Sterling amesisitiza kuwa anahitaji kuonesha kiwango kikubwa katika klabu yake ya Liverpool msimu ujao.
Nyota huyo kinda mwenye miaka 19 alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Liverpool waliokaribia kutwaa ubingwa wa ligi kuu ambapo walimaliza pointi mbili nyuma ya mabingwa Manchester City.
Sterling amejiunga na kambi ya mazoezi iliyopo Boston akijua wazi kuwa kusajiliwa kwa wachezaji wapya kunamaanisha nafasi yake haina uhakika.
Akizungumza na LFCTour.com, alisema: "Bado natakiwa kujithitisha mwenyewe, kocha ameleta wachezaji ambao wenye uwezo wa kucheza nafasi kama yangu, natakiwa kumuonesha kocha na kujituma zaidi ili kupata namba ya kudumu katika timu".
Fast tracked: Raheem Sterling has developed rapidly since Liverpool last visited Boston
Kivutio: Raheem Sterling amekuwa na mvuto tangu alipowasili katika kambi ya Liverpool iliyopo Boston.

"Hii ni klabu ya juu ikiwa na wachezaji wa kiwango cha juu, ambao wamekuja kushindana siku zote. Hakuna utofauti sana kwenye mazoezi"
"Kuna vitu vingi kutoka kwangu. Nahitaji kujituma na natumaini nitapata namba msimu ujao na kufanya kila linalowezekana kuisaidia klabu".
Sterling alijitambulisha mwenyewe katika ulimwengu wa soka baada ya kuonesha kiwango cha huu kwenye mechi ya ufunguzi ya kombe la dunia dhidi Italia ambapo walilala mabao 2-1, lakini kijana huyo mwenye kipaji alicheza mpira mwingi mno.
Competition: Signing of new players including Lazar Markovic (L) will keep pressure on Sterling
Ushindani: Wachezaji wapya waliosajiliwa ni pamoja na Lazar Markovic (kushoto) ambao watampta presha Sterling
Gruelling: Raheem Sterling takes on England teammate Daniel Sturridge during double training in Boston
Raheem Sterling akichuana na mchezaji mwenzake wa England  Daniel Sturridge wakati wa mazoezi  Boston.

0 comments: