Imechapishwa Julai 22, 2014, 2014, saa 4:26 asubuhi
ALVARO
Morata ameanza kwa majanga katika klabu yake mpya ya Juventus baada ya kupata
majeraha ya goti kwenye mazoezi ya kwanza.
Mshambuliaji
huyo wa Kihispania mwenye miaka 21 alijiunga na mabingwa hao wa Seria A siku ya
jumamosi kutokea klabu ya Real Madrid.
Nyota huyo
alijigonga kwenye mazoezi na alikuwa analalamika maumivu ya goti na kwasasa
kinachosubiriwa ni majibu ya vipimo.
“Kwenye
mazoezi ya mchana huu (jana), Alvaro Morata ameripotiwa kupata majereha ya goti”.
Juventus walithibitisha kwenye mtandao wao rasmi. “Hali yake itatathiniwa kesho
(leo)”.
Morata
anatarajia kupewa matibabu ya haraka ili atulie katika klabu ya Juve na kupamba
na Carlos Tevez na Fernando Llorente kwenye kikosi cha kwanza cha Massimiliano
Allegri.
Kocha huyo alirithi mikoba ya Antonio Conte jumatano na Morata ndiye mchezaji wa kwanza kumsajili na atarajia kuendeleza mafanikio klabuni hapo.
0 comments:
Post a Comment