Na Mahmoud Ahmad Mwanga .
WANANCHI wanaoishi ukanda wa Ziwa Jipe wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro
wamelalamikia kukabiliwa na umaskini unaochangia kutoweka kwa ziwa hilo
ambalo sehemu kubwa limefunikwa na
magugu na wameomba serikali kufanya kila linalowezekana kushughulikia tatizo hilo.
Wananchi hao ambao asilimia kubwa ni wa
Tarafa ya Jipendea ambao ndio walioko mpakani na
ziwa hilo wamesema tatizo la magugumaji linaendelea kuongezeka hasa kwa
upande wa Tanzania na licha ya kutishia
kutoweka kwa ziwa hilo yamesababisha kuongezeka kwa makali ya maisha hasa
kwa vijana waliokuwa wanaishi kwa kutegemea uvuvi.
wananchi hao akiwemo Bw, Rashidi K idundi ambaye ni Afisa mtendaji kata ya
Jipe amesema tatizo hilo linawaathiri zaidi vijana ambao kutokana na kukwama kwa shughuli za uvuvi wanakosa
uvumilivu na kujikuta wakiingia upande wa pili wa ziwa hilo ambao uko nchini Kenya kuendesha uvuvi
haramu na kuishia mikononi mwa polisi.
Bw kidundi ameongeza kuwa hali hiyo imesababisha viujana wengi kukamatwa na
kufunguliwa mashtaka nchini Kenya na kwamba hadi sasa vijana wanne wamehukumiwa
na wamefungwa katika magereza ya nchi hizo.
“Pamoja na kwamba ni Kinyume cha
sheria lakini kuna vijana wamekamatwa na kufungwa nchini Kenya
tumejaribu kufuatilia kupitia kamati za ulinzi na usalama lakini bado na tumeshamweleza
mkuu wa wilaya na anasema anaendelea kulishughulikia”
Naye Bw, Yusuph Ramadhani na
Bi Zukra Mohamed wamesema tatizo hilo pia limeoangeza uharibifu
wa mazingira kwani vijana wengi wanalazimika kujiingiza katika ukataji wa miti na kulima katika
maeneo ya miinuko na vyanzo vya maji.
Akizungumzia changamoto hiyo waziri wa maji Mh Prf Jumanne Maghembe ambaye pia ni mbunge wa
Mwanga amesema wataalam wa ndani na nje
wanaendelea kushughulikia tatizo hili na amewataka wanachi kuendelea kuheshimu sheria hasa
za uvuvi kwani kuzikiuka ni kuongeza matatizo.
Ni kweli kuna tatizo la magugu katika ziwa hili na
maziwa mengine laikini serikali haijakaa kimya bado
inaendelea kutafuta ufumbuzi kwa kushirikiana na wataalam kutoka
nchi mbalimbali lakini
cha msingi hapa ninachowaomba ni kuwa muendelee kufuata sheria hasa za zinazosimamia uvuvi kwani kuzivunja
sio suluhu ya matatizo “alisema Prf Maghembe waziri wa maji na pia Mbunge wa Mwanga
Kwa muda mrefu sasa ziwa jipe limekuwa katika changamoto kubwa ya kufunikwa na
Magugu na licha ya kuwepo kwa jitihada za
wataalam wa ndani na nje wa kuyakabili hadi sasa bado tatizo ni kubwa na kama lingeweza
kupata ufumbuzi licha ya kuwawezesha wananchi wa
ukanda huo kiuchumi na pia kuongeza hata pato la taifa kupitia uvuvi .
0 comments:
Post a Comment