Mtu aliyezoeleka: Dunga ameteuliwa kwa mara ya pili kuwa mirthi wa Luiz Felipe Scolari.
Imechapishwa Julai 22, 2014, saa 12:34 jioni
BRAZIL imemtangaza Dunga kwa mara ya
pili kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya Luis Felipe
Scolari kuachishwa kazi kutokana na kipigo cha mabao 7-1 kwenye mechi ya
nusu fainali ya kombe la dunia dhidi ya Ujerumani na 3-0 katika mechi
ya mshindi wa tatu na Uholanzi.
Tangazo rasmi limetolewa leo jumanne na sasa kocha huyo mwenye miaka 50 anaanza kazi ya kuwanoa Samba Boys.
Kwa mara ya mwisho Dunda aliyewahi kuwa
nahodha wa Brazil mwaka 1994, aliifundisha Brazil katika fainali za
mwaka 2010 nchini Afrika kusini na alifukuzwa baada ya kushindwa kufuzu
zaidi ya robo fainali.
"Kiukweli nina furaha kubwa kurudi tena," aliwaambia waandishi wa habari.
Miaka ya nyuma: Dunga aliingoza Brazil mpaka hatua ya robo fainali ya kombe la dunia nchini Afrika kusini.
0 comments:
Post a Comment