Saturday, 2 August 2014

Gaza:Mashambulizi ya Israel yawaua 100


 
Gaza

Maafisa wa matibabu katika eneo la Gaza wanasema kuwa zaidi ya wapalestina 100 wameuawa na makombora ya Israeltangu kukiukwa kwa makubaliano ya kusitisha vita siku ya ijumaa.
Vifo vingi vimetokea katika eneo la Rafah kusini mwa Gaza ambapo wanajeshi wawili wa Israel waliuawa na mwengine wa tatu kudaiwa kutekwanyara baada ya kuvamiwa na wapiganaji wa Hamas.
Kundi la wapiganaji wa kipalestina Hamas limesema kuwa halina habarizozote kuhusu mwanajeshi aliyetoweka Hadar Goldin na kwamba huenda aliuawa katika mapigano.

 

0 comments: