Na Magreth Kinabo, DODOMA
Chama cha Wakulima Wadodowadogo wa
zao la Pamba Tanzania(TACOGA) kimemwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe . Dkt . Jakaya Mrisho Kikwete asisitishe mchakato wa
mijadala ya Bunge Maalum la Katiba , kwani kitendo cha kusitisha ni
kuzuia makusanyo ya mawazo mtambuka ya wabunge .
Kauli hiyo imetolewa leo na
Katibu chama hicho, George Mpanduji wakati akizungumza na
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta Maalum ofisini
kwake mjini Dodoma leo kwa lengo la kuwasilisha Azimio la wito wa
kuomba Bunge Maalum la Katiba kukamilisha jukumu la kuandaa rasimu
yenye kuzingatia haki ardhi kwa mahitaji ya wakulima Tanzania.
Mpanduji aliambatana na baadhi wa
viongozi na wajumbe kutoka mikoa 11 wa TACOGA ,alisema wanaheshimu
makubaliano ya kisiasa ya kutungwa Katiba ya Nchi, lakini
tunatahadharisha kuwa shurti za kisiasa zinazopiganiwa na vyama vya
upinzani Bungeni hadi kuzuia wabunge kutetea haki mtambuka za kijamii
suala hilo linaleta hitilafu ya kuchelewesha mahitaji muhimu kama ya
kujengwa amani kati ya wakulima na wafugaji.
“ Vikao vya Bunge Maalum
viendelee na wabunge wote watangulize kwanza maslahi ya umma dhidi ya
misukumo batili iliyo kinyume na maslahi mapana ya umma na taifa.
Wabunge hawa wanafikra chanya za kujenga makutano ya fikra patanifu ya
kupatikana suluhu za haki za makundi mbalimbali, hususani pale palipo na
ombwe la matakwa hayo Katika ya sasa,” alisema Mokiri.
Aidha Mpanduji aliongeza kwamba
wanashauri agenda za haki mbalimbali kwa jamii zipewe vipaumbele kwa
kuwa pana vilio vya kuhitajika suluhu za haraka kwa mahitaji mbalimbali
ya makundi ya umma.
Mpanduji alisema wakulima hao,
wanataka Katiba ipatiokane haraka kwani itakuwa suluhisho dhidi ya
mizozo na maafa yanayotokea nchni kati ya wakulima na wafugaji.
“ Tunahimiza vyama vya siasa
vishindanishe hoja za kukonga mioyo kwa kutetea haki za jamii na taifa
dhidi ya kutambulisha misukumo y shurti za utashi wa makundi ya watu ya
maslahi binafsi,” alisisitiza.
Alisema chama hicho ,pia
kinampongeza Mhe. Sitta kwa uvumilivu wake na hekima ya uongozi na
wabunge wote wanaohudhuria vikao vya Bunge hilo kwa kuwa wanatimiza
uzalendo wao, uaminifu wao na utiifu wao wa kutumikia jamii na taifa.
Chama hicho kimtaka mlezi wao
ambaye ni John Shibuda Mbunge wa Jimbo la Maswa Maghribi, ambaye
waliochagua kuanzia mwaka 2012 kuendelea kuhudhuria vikao vyote vya
Bunge hilo ili akasimamie maslahi yao na aungane na vikundi vinavyoandaa
na kutetea haki za wakulima Tanzania.
Kwa upande wake Mhe. Sitta alisema lengo la kutungahiyo ni iwe rafiki yenye kukidhi matakwa ya wananchi.
Miongoni mwa hoja nyingine
walizozungumzia ili Katiba itamke ni haki ya mikopo kwa wakulima, ruzuku
wa wakulima, iwalinde na itamke haki za wanawake katika kumiliki ardhi
wanapofiwa na waume zao na kufadika na mapato ya kilimo.
0 comments:
Post a Comment