Kutokana na presha ya usalama kuwa mdogo
wakati wa mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga, Bodi ya Ligi imeamua
kuongeza askari wa usalama hadi 400 kwa ajili ya kulinda amani siku watani hao
watakapokutana.
Hayo yamesemwa na ofisa mtendaji wa bodi hiyo,
Silas Mwakibinga, ambaye amesema kuwa wameamua kuongeza idadi ya askari hadi
kufikia 400 ambao watakuwa na vitendea kazi kama farasi na mabomu ya machozi
kutokana na vitendo vya fujo ambavyo vimekuwa vikijitokeza katika mechi za
watani.
Simba kwa sasa ipo chini ya kocha Mzambia,
Patrick Phiri huku Yanga ikiwa chini ya Mbrazil, Marcio Maximo.
“Tanzania
hatujafikia hatua ya kufungia mashabiki. Kwanza fujo za mashabiki wetu si za
kuhatarisha maisha ya wachezaji kama nchi nyingine, mfano Misri, pili ‘nature’
ya mpira wetu ni wa kutegemea viingilio, hivyo tumeamua kuboresha sekta ya
ulinzi msimu huu kwenye mechi kubwa,” alisema Mwakibinga.
0 comments:
Post a Comment