Wanawake waliotaka kuandamana
mkoani Arusha mandamano yao ya yayeyuka katika mazingira ya
kutatanisha,maandamano yaliyopangwa kufanyika jana kupinga mauaji
waliyodai kuwa ya wanawake wanaoendesha magari pekee yameyeyuka kutokana
na kutojua nani anayeratibu na ushahidi wa wanawake wanaodaiwa kuuawa
yaliokuwa yafanyike jijini hapa.
Mauaji hayo yanaelezwa
kutekelezwa na watu wanaotumia usafiri wa bodaboda kwa kumfuata mwanamke
anayeendesha gari na kisha kumsimamisha na pindi anapofungua kioo cha
gari wanamfyetulia risasi pasipo kupora kitu chochote.
Maandamano hayo yaliyopangwa
kufanyika kuanzia majira ya saa nne asubuhi kwa wanawake hao kukutana
katika jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha pia yalikosa nguvu
kutokana na kutoelezwa mahali pa kuanzia wala saa ya kukutana.
Taarifa za kuwataka wanawake hao
kuandamana zilitolewa kwa njia ya mtandao wa kijamii ambao ulisambaa
katika simu za mikononi uliokuwa ukihamasisha kila mwanamke na wasichana
jijini Arusha kujitokeza kwa wingi katika maandamano hayo kama hatua ya
kupinga mauaji hayo waliyodai kuwahusu wanawake wanaoendesha magari.
Kuhusu wanawake hao kukosekana
kwa ushahidi wa mauaji hayo kunatokana na maswali yaliyoulizwa na
kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas kwamba wanawake
waliouawa ni wapi kutokana na taarifa za kuwepo kwa wanawake sita
waliouawa katika matukio hayo.
Kamanda Sabas hapo juzi alipokua
akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na taarifa hizo za uzushi
alisema ni mwanamke mmoja tu Shamimu Yulu ndiye aliyeuawa kwa kupiwa
risasi maeneo ya Sakina Kwa Idd mnamo mwezi huu tena katika tukio la
uporaji wa kawaida kwa kutumia silaha na siyo kama inavyoelezwa kuwa
lengo ni kuua wanawake wanaoendesha magari.
Kamanda Sabas alitaja tukio
lingine la mauaji ya kutumia silaha yaliyotokea kipindi hichi kuwa ni
lile lililohusisha kifo cha mtoto wa miaka mitatu maeneo ya Olasiti
baada ya watu waliokuwa na bodaboda kumsimamisha baba aliyekuwa
akiendesha gari na kisha kukataa na ndipo walipofyetua risasi iliyompata
mtoto huyo na kisha kupora shilingi 2000.
Mapema leo asubuhi wanawake
wachache walionekana wakiwa katika vikundi vikundi katika maeneo ya
hoteli ya Goldenrose,Bwalo la maafisa wa polisi jijini hapa na wengine
wakiwa wamejificha katika magari yao maeneo ya ofisi ya mkuu wa mkoa
wakiangalia iwapo kuna wenzao waliojitokeza.
Hata hivyo polisi wa FFU
walionekana katika baadhi ya maeneo ya mji wakipitapita kuona iwapo
kutakuwa na maandamano hayo ambayo hata hivyo jeshi la polisi liliyazuia
kwakua hayakuwa na ukweli wowote wala kibali.
Hata hivyo jana mkuu wa mkoa wa
Arusha katika mkutano wake na waandishi wa habari aliwata wanawake
mkoani Arusha kusitisha maandamano hayo kwakua vyombo vya ulinzi na
usalama vimeingia kazini na mapema
Kamanda Sabas akizungumzia
matukio hayo alisema tayari watuhumiwa saba wameshakamatwa na wawili
kati ya wameshafikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo wakati wengine watano
wakiendelea kuhojiwa na msako mkali dhidi ya wengine waliobaki
ukiendelea.
NA MAHMOUD AHMAD,ARUSHA.
0 comments:
Post a Comment