Tuesday, 26 August 2014

KAULI YA CCM KWA WAZIRI MKUU KUGOMMBEA URAISI


NAPE_4672d.jpg
Nchini Tanzania Chama tawala CCM kimesema kuwa kitafanya uchunguzi wa kina ili kujiridhisha kabla ya kuchukua hatua dhidi ya Waziri mkuu wa nchi hiyo Mizengo Pinda iwapo matamshi yake ya kutangaza nia ya kuwania Urais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi mkuu hapo mwakani uliambatana na vitendo vya kufanya Kampeini.Awali chama hicho kiliwahi kuwaonya baadhi ya vigogo kadhaa ambao walionyesha kuanza kufanya kampeini mapema ambapo sasa kufuatia hatua ya Kigogo huyo ambaye ni Waziri mkuu aliyeko madarakani inaanza kufungua mwanya katika mbio za kuelekea Ikulu hapo mwakani.Erick David Nampesya amezungumza na Katibu wa Itikadi wa CCM Nape Nnauye ameanza kwa kusema kutangaza nia ya kuwania Urais siyo kosa kisheria

0 comments: