Na Magreth Kinabo, Dodoma
Rais wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ameahidi
kuonana na Viongozi wa Vyama vya Siasa vinavyounda Kituo cha Demkrasia
Tanzania(TCD) kabla ya mwisho wa wiki kwa lengo la kushauriana.
Kauli hii
imetolewa na Mwenyekiti wa TCD,Mhe. John Cheyo mjini Dodoma wakati
akizungumza na waandishi wa katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Bunge.
Mhe.
Cheyo alisema Rais Kikwete amekubali kuonana nao kufutia kikao chao
walichokaa kwa pamoja ambacho kilihusisha viongozi wakuu wa vyama hivyo,
Agosti 23,mwaka huu, ambapo walijadili na kutafakari maendeleo ya
mchakato wa Katiba Mpya.
Alisema
viongozi hao, katika kiako hicho cha pamoja na mambo mengine waliazimia
kutafuta nafasi ya kuonana na Rais Kikwete kwa ajili ya lengo hilo,
ambapo kufutia azimio hilo, Mwenyekiti huyo aliwasiliana naye alilipokea
azimio hilo na kuahidi kufanya hivyo.
"Tutalishauri taifa kwa maoni tutakayokubaliana na Rais," alisema Mhe. Cheyo bila ya kutaja agenda juu ya jambo hilo.
Aliongeza kuwa watazunguza na kutafakati ili kuhimarisha amani na mchakato huo utoe matunda mema.
Mhe. Cheyo alisema kikao hicho kilifanyika na kuhusisha vyam vyote vilivyoko katika TCD.
Alisema hii ni mara ya kwanza kwa TCD kumwomba Rais Kikwete kuonana naye na kukubali ombi hilo.
0 comments:
Post a Comment