Mwanahamisi
Omary (26) alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Hassan Juma kuwa
alimfahamu mganga huyo baada ya kusumbuliwa na tumbo la uzazi kwa muda
mrefu.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali Felista Mosha,
Mwanahamisi alidai alikuwa akitibiwa ugonjwa huo bila ya kutoa taarifa
kwa mumewe Edrick Elinezer. Alidai alitibiwa kwa miezi sita bila ya
mafanikio.
Shahidi huyo alidai Aprili, mwaka
huu, Michael alimwambia kuwa ana majini hivyo hawezi kupata mtoto na
kumpatia dawa kwa ajili ya kunywa na kuoga.
Alidai
mganga huyo alikuwa akimtibu nyumbani kwake lakini baadaye alihamishia
ofisi yake katika nyumba ya kulala wageni iliyopo Kigogo Luhanga na
kudai kuwa mganga huyo alikuwa akipaka dawa katika uume wake na
kumuingilia kimwili huku akiwa hajitambui kwa madai kwamba atamsaidia
kupata mtoto.
Aliendelea kudai kwamba baada ya
kutokuwa na mawasiliano kwa muda mrefu na mumewe, alipata taarifa kuwa
mume wake alipigiwa simu na mganga huyo na kumtaka apeleke gari lake
Toyota Rav4 lenye namba za usajili T 139 BSG maeneo ya Jangwani kwa kuwa
majini ya mkewe yanataka mtoto.
Awali, Hakimu
Juma alisema wadhamini wa mshitakiwa wanatakiwa kumtafuta mshitakiwa
huyo na kumfikisha Mahakamani hapo, aliwatahadharisha wasipofanya hivyo
kwa wakati watalipa faini ya Sh milioni sita kwa kila mmoja.
Michael
alidaiwa Aprili 29, mwaka jana, maeneo ya Jangwani Wilaya ya Ilala,
alijipatia gari aina ya Toyota Rav4 T 139 BSG lenye thamani ya Sh
milioni 12 mali ya Eliezer kwa njia ya udanganyifu. Kesi hiyo
itasikilizwa tena Septemba 18, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment