Mechi
nyingine ya tiketi za elektroniki siku hiyo itachezwa Uwanja wa Kaitaba
mjini Bukoba kwa kuzikutanisha timu za Kagera Sugar na Geita Gold SC ya
mkoani Geita. Geita Gold iko Daraja la Kwanza
Kabla
ya mechi hizo, Ijumaa (Agosti 29 mwaka huu) saa 3 asubuhi kwenye
viwanja hivyo kutakuwa na mafunzo ya matumizi ya tiketi za elektroniki
pamoja na jinsi mfumo huo unavyofanya kazi.
Washiriki
wa mafunzo hayo ni wasimamizi wa vituo vya Tanga na Bukoba, viongozi wa
vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (KRFA) na Tanga (TRFA),
makatibu na maofisa habari wa klabu za Kagera Sugar, Mgambo Shooting,
African Sports na Geita Gold, mameneja wa viwanja vya Kaitaba na
Mkwakwani na wasaidizi wao, maofisa usalama wa TRFA na KRFA, wachanaji
tiketi, wasimamizi wa milangoni, wasaidizi (stewards) na waandishi wa
habari.
Thursday, 28 August 2014
HOME »
» MECHI ZA TIKETI ZA ELEKTRONIKI KUPIGWA TANGA, BUKOBA.
0 comments:
Post a Comment