HOME »
» BURUNDI YACHUNGUZA MIILI ILIYOPATIKANA ZIWANI
Mamlaka kaskazini mwa Burundi
zimeanzisha uchunguzi baada ya mifuko yenye miili ya binaadam kupatikana
ikielea katika ziwa Rweru lililopo kwenye mpaka na Rwanda. Wavuvi
katika eneo hilo wamesema miili ya watu wasiofahamika imekuwa ikionekana
katika ziwa hilo katika wiki za hivi karibuni. Haifahamiki watu hao
walikufa katika mazingira gani. Polisi nchini Rwanda wametoa taarifa
ikikanusha kuwa miili hiyo ni ya raia wake waliouawa na kutupwa ziwani.
0 comments:
Post a Comment