HOME »
» LAMPARD ASTAAFU RASIMI SOKA LA KIMATAIFA
Frank Lampard ametangaza kustaafu
kucheza soka la kimataifa. Kiungo huyo, aliyejiunga na Manchester City
kwa mkopo akitokea New York City, alicheza mechi yake ya mwisho kama
nahodha wa England katika sare ya 0-0 dhidi ya Costa Rica katika
michuano ya Kombe la Dunia, mwezi Juni. Kiungo huyo wa zamani wa
Chelsea, 36, ameichezea timu yake ya taifa mara 106, tangu Oktoba mwaka
1999, alipocheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Ubelgiji. Lampard
amecheza katika michuano mitano mikubwa na kupachika mabao 29. Anakuwa
mchezaji wa sita kuwahi kuichezea England mara nyingi zaidi sawa na Sir
Bobby Charlton. Lampard, aliyeanza kucheza soka la kulipwa katika klabu
ya West Ham, aliondoka Chelsea msimu uliopita baada ya kuichezea klabu
hiyo mara 648 na kufunga magoli 211
0 comments:
Post a Comment