JAMALI MALINZI RAIS WA TFF |
Kumbukumbu
ya Karume, Ilala ili yawe katika kiwango cha kisasa ikiwa ni pamoja na
kuwa na vitendea kazi na miundombinu ikiwa ni pamoja na upanuzi wa
ofisi.
Hatua
hiyo itaiwezesha TFF kuwa na mazingira bora ya kufanya shughuli zake
kwa ufanisi. Vilevile kupitia programu zake mbalimbali ikiwemo ile ya
Goal, FIFA imeahidi kushirikiana na TFF katika kuendeleza mradi wa
kiuchumi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Mwanzoni
mwa mwaka huu, TFF ilihamishia makao yake makuu katikati ya jiji ili
kupisha maendeleo ya kuiwezesha Karume kuwa kituo cha kisasa kwa
michezo na vitega uchumi.
Akiongea
mwishoni mwa ziara ya kikazi nchini, Meneja Miradi wa FIFA
anayeshughulikia Programu za Afrika, Zelkifli Ngoufonja amesema FIFA
inaunga mkono wazo la kuboresha makao makuu ya Karume na itasaidia kwa
awamu uboreshaji huo.
Katika kuhakikisha usimamizi na utekelezaji
barabara
wa mradi huo, ujumbe huo wa FIFA ulikubaliana na Kamati ya Utendaji ya
TFF kuboresha ofisi za Karume ili jengo la utawala lianze
kutumika huku mradi ukitekelezwa kwa awamu.
Pamoja
na kuongelea mradi huo muhimu kimichezo na kibiashara, ujumbe huo
uliokuwa nchini kwa juma moja kufuatia mwaliko wa TFF ulikuwa na nafasi
ya kujadiliana na TFF kuhusu maboresho katika masuala mbalimbali
yakiwemo ya
Utawala, Fedha, Masoko, Ufundi, Mashindano na timu za taifa.
Akiongea
kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya TFF, Rais wa TFF Jamal Malinzi
aliushukuru ujumbe huo wa FIFA kwa msaada mkubwa katika historia ya
mahusiano kati ya FIFA na TFF.
Ujio
huo unafuatia maombi ya TFF kuwa sehemu ya mradi wa Performance wa
FIFA. Mradi wa Performance unaoshirikisha nchi mashirikisho 163 kati ya
wanachama 209 wa FIFA, unalenga kuongeza ufanisi katika uendeshaji na
uongozi wa nchi wanachama wa FIFA.
Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
0 comments:
Post a Comment