Jeshi la Polisi mkoani
Mtwara limefanikiwa kuokota milipuko 10 iliyotengenezwa kienyeji ambayo
ilikuwa imetelekezwa jirani na Shule ya Msingi Raha Leo na Sekondari ya
Raha Leo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Augustino Ollomi
alieleza kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 11 na kwamba waliweza
kuibaini milipuko hiyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
Alisema kuwa baada ya polisi kupata taarifa,
ilichukua hatua za haraka ikiwa ni pamoja na kufika eneo la tukio na
kufanikiwa kuokota milipuko kumi iliyotengenezwa kienyeji.
Kamanda Ollomi alibainisha kuwa mabomu hayo
yalitengenezwa kwa kutumia chupa za plastiki zenye ujazo wa nusu lita
zilikuwa zimejazwa mbolea ya urea,
iliyochanganywa na mafuta ya taa huku
zikiwa zimefungwa pamoja na urojo wa baruti, waya wa kulipua na chuma
cha kulipua zipatazo saba zikiwa zimefichwa kichakani jirani na zilipo
shule.
0 comments:
Post a Comment