Wednesday, 27 August 2014

AUWAWA KWA KOSA KUIBA SIMU YA ELFU 25 MKOANI

 

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

 images
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA IBUNGU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DAUD PASTON (22) ALIUAWA KWA KUKATWA NA VITU VYENYE NCHA KALI SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA KATIKA MTO LUMBE.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NA KUTOLEWA KATIKA MTO LUMBE ULIOPO KATIKA KIJIJI NA KATA YA IKUTI, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA MNAMO TAREHE 26.08.2014 NA ULIKUTWA NA MAJERAHA SEHEMU MBALIMBALI YA KUCHOMWA/KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI.
CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO HAKIJAFAHAMIKA JAPO TAARIFA ZA AWALI ZINADAI KUWA MAREHEMU ALIKUWA NA TABIA YA WIZI NA UBAKAJI. HAKUNA MTU/WATU WALIOKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO NA JITIHADA ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FRANK MWAKILALO (25) MKAZI WA BLOCK T ALIFARIKI DUNIA AKIWA ANAPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA BAADA YA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA TUHUMA ZA KUIBA SIMU YENYE DHAMANI YA SHILINGI ELFU 25.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.08.2014 MAJIRA YA SAA 20:15 USIKU HUKO KATIKA MAENEO YA BLOCK T, JIJI NA MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKAMATWA NA KUANZA KUPIGWA NA WANANCHI HAO NA BADAE ALIPELEKWA NA KUFUNGIWA KATIKA OFISI ZA MTENDAJI AMBAPO ALITOROKA NA NDIPO WANANCHI HAO WALIMUONA NA KUMKIMBIZA NA KUANZA KUMPIGA HALI ILIYOPELEKEA KUMVUNJA MKONO WAKE WA KUSHOTO NA KUMSABABISHIA MAUMIVU MAKALI MWILINI.

HAKUNA MTU/WATU WALIOKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILO ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA MAKOSA/TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

KATIKA TUKIO LA TATU:
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 09 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NELLY ALICK MKAZI WA MLOLO AMEFARIKI MUDA DUNIA MUDA MFUPI WAKATI ANAPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.257 CRP AINA YA TOYOTA NOAH LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA LAMECK MADIHAN (34) MKAZI WA MLOLO.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 26.08.2014 MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI HUKO MAENEO YA KARASHA, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA MBOZI. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA, ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUWA MAKINI WANAPOTUMIA BARABARA ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

0 comments: