Polisi nchini Marekani
wameshindwa kumkamata balozi wa Equatorial Guine mjini Washngton, kwa
tuhuma za kumpiga binti yake kwa mguu wa kiti cha mbao, balozi huyo
hajakamatwa mpaka sasa kutokana na kinga yake ya kibalozi alonayo .
Msemaji wa polisi Dustin Sternbeck amesema
kwamba walipewa taarifa mapema wiki hii kua kuna tukio nyumbani kwa
balozi huyo, na walipofika wakamkuta binti huyo mdogo akiwa na jeraha
kubwa kichwani mwake ambaye alihitaji tiba na hivyo kumpeleka
hospitalini kwa matibabu.Pamoja na hayo yote Dustin alisema kua polisi hawana mamlaka kwa kesi za namna hiyo zinazowahusisha wanadiplomasia lakini wamekwisha iarifu serikali juu ya suala hilo.
0 comments:
Post a Comment