KLABU ya Everton imetangaza kumsajili mshambuliaji Mcameroon, Samuel Eto'o kwa mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru.
Mpachika
mabao huyo mwenye umri wa miaka 33 alitemwa na Chelsea mwishoni mwa
msimu uliopita na amejiunga na Toffees kufuatia mango wa kuhamia kwa
majirani zao, Liverpool kukwama.
Liverpool
ilitaka kumsajili Eto'o iwapo ingemkosa Mario Balotelli, lakini baada
ya kumnasa Mtaliani huyo, dili hilo limekufa kifo cha kawaida.
Mshambuliaji
huyo wa zamani wa Barcelona ametweet; "Rasmi ni mchezaji wa
Everton...!!! Acha niwe tayari kwa matarajio na changamoto mpya!!!'
0 comments:
Post a Comment