Sunday, 24 August 2014

MHE.SITTA AZUNGUMZA NA WAKULIMA WA PAMBA

0D6A6917Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akizungumza na baadhi  viongozi na wajumbe kutoka Chama cha Wakulima Wadodowadogo wa zao la Pamba Tanzania(TACOGA) katika ukumbi wa mikutano wa Bunge wa Pius Msekwa leo wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma  kwa lengo la  kuwasilisha Azimio la wito wa kuomba Bunge Maalum la Katiba  kukamilisha jukumu la kuandaa rasimu yenye kuzingatia haki ardhi kwa mahitaji ya wakulima  Tanzania.
0D6A6935 
Kaimu Mwenyekiti wa kutoka Chama cha Wakulima Wadodowadogo wa zao la Pamba Tanzania(TACOGA), Godfrey  Mokiri(katikati) akizungumza  na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta(kulia)  katika ukumbi wa mikutano wa Bunge wa Pius Msekwa leo wakati  baadhi  viongozi na wajumbe wa chama hicho  walipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma  kwa lengo la  kuwasilisha Azimio la wito wa kuomba Bunge Maalum la Katiba  kukamilisha jukumu la kuandaa rasimu yenye kuzingatia haki ardhi kwa ardhi kwa mahitaji ya wakulima  Tanzania.Kushoto ni Katibu wa chama hicho, George Mpanduji.
0D6A6980 
Baadhi  viongozi na wajumbe wa  Chama cha Wakulima Wadodowadogo wa zao la Pamba Tanzania(TACOGA) wakiwa katika picha ya pamoja  na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta (wanne kushoto) na Katibu wa Bunge hilo, Yahaya Khamis Hamad (wa tatu kulia )walipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma leo kwa lengo la  kuwasilisha Azimio la wito wa kuomba Bunge Maalum la Katiba  kukamilisha jukumu la kuandaa rasimu yenye kuzingatia haki ardhi kwa mahitaji ya wakulima  Tanzania.

0 comments: