Saturday, 23 August 2014

KIKONGWE WA MIAKA 76 AAMUA KUJITENGENEZEA JENEZA KWA SABABU YA UGUMU WA MAISHA


Bi
Scholastika Mhagama akiwa katika mlango wa nyumba yake.
 ———————

Wahenga walisema Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni;’ Jamii inazidi kujawa na chuki naukatili ndani yake, imekuwa kawaida siku hizi kusikia fulani kamuua fulani kwakisa kisichokuwa na maana.Maalbino wanakatwa viungo vyao kwa visingizio vya
kupata utajiri kwa watu wasiokuwa na huruma, watoto wadogo wananyimwa haki zao na kuwekwa ndani ya maboksi na wengine kuishi maisha yao katika uvunguza
kitanda yote haya ni mambo ya kutisha yanayotendeka katika jamii zetu.
Hali imekuwa tete amani na upendo vinazidi kuyeyuka
kama barafu, watu hawana utu tena, wamejivika ngozi za kondoo wakati mioyo yao ni ya Simba, hakuna tena roho ya huruma kwa wanadamu wa dunia ya leo.
Choo cha bibi Scholastika Mhagama
Jeneza la bibi likitolewa ndani kwake na wanachama wa Kombination Camp
 Jeneza la Bi Scholastika Mhagama
 
Akielezea historia ya maisha yake Bi Scholastika
anasema alizaliwa akiwa na miguu yote lakini alipata bahati mbaya ya kugongwa
na nyoka alipokuwa darasa la pili hali iliyomfanya kukatwa mguu ili kuepusha
madhara mengine kama vile kifo. Hivyo maisha yake yalibadilika na tangu hapo
akawa mlemavu.
 Hali hiyo ya
ulemavu lakini pia uzee alionao vimemfanya ashindwe kujihudumia kwa lolote
zaidi ya kupika tu. Hata hivyo anakosa mahitaji muhimu kama vile maji na chakula
hali inayomfanya alale na njaa kwa baadhi ya siku.
Kwa hali aliyo nayo ni wazi kuwa Bi Scholastika
anahitaji baiskeli ya miguu mitatu (wheel chair) ambaye itamwezesha  kutembea
kwa kuwa hivi sasa anatambaa na kupata maumivu makali kutokana na nyama
iliyobakia kwenye nyonga baada ya kukatwa mguu.
Bi Scholastika anazidi kueleza kuwa kuna watu waliwahi
kufika kumuandikisha jina lake na kumuingiza katika orodha ya watu wanaostahili
kupata msaada lakini anasikia misaada inafika kwa jina lake lakini yeye
mwenyewe hajawahi kuipata.
Vipi kuhusu Sera ya Wazee?
Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003
inaweka bayana kuwa suala la uzee na kuzeeka limekuwa lenye umuhimu mkubwa
ambapo karne ya ishirini imeshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya wazee.
Kwa kurejelea takwimu zilizopo ni kwamba, ifikapo
mwaka 2050 idadi ya wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60 nchini hapa
itaongezeka na kufikia wazee milioni 8.3 (Sawa na asilimia 10 ya watanzania
wote)
Kama hiyo haitoshi, Taarifa ya Umoja wa Mataifa ya
mwaka 1999 inaeleza kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wazee duniani
na kwamba ongezeko hilo linaonekana zaidi katika nchi zinazoendelea (Tanzania
ikiwepo) ambapo viwango vya ongezeko hilo havilingani na uwezo wa rasilimali
zilizopo za kuwahudumia.
Rasilimali hizo zinajikita zaidi katika Nyanja za
msingi katika makuzi ya binadamu yoyote zikiwemo Nyanja za afya, lishe na
huduma nyingine za msingi zisizoweza kuepukwa na binadamu yeyote.
 
 Na Oswald Ngonyani wa demashonews
– Peramiho.

0 comments: