Mechi kubwa: Manuel Pellegrini asema mechi dhidi ya Liverpool ni muhimu mno.
KOCHA wa Manchester City, Manuel
Pellegrini ameweka wazi kuwa kamwe hakuwahi kuihofia Liverpool katika
mbio za ubingwa msimu uliopita.
Kuelekea katika mtanange wa jumatatu
dhidi ya Liverpool katika dimba la Etihad, Mchile huyo alisema kikosi
cha Brendan Rodger kitakabiliwa na presha kubwa mpaka kufikia mwezi mei
mwaka huu.
Msimu uliopita, Liverpool walipanda
kileleni mwezi aprili mwaka huu baada ya kuifunga City mabao 3-2 katika
dimba la Anfield, lakini msimu ulimalizika kwa machozi baada ya wakali
hao wa Pellegrini kuwazidi kete mwishoni na kutwaa ubingwa.
Katika msimu huo,makosa ya nahodha Steven
Gerrard yalichangia kufungwa na Chelsea wakiwa nyumbani na wiki moja
baadaye walitoka sare ya 3-3 na Crystal Palace katika dimba la Selhurst Park na kuzika matumaini ya ubingwa.
Mambo yalikuwa tofauti kwa City kwasababu walishinda mechi zote tano za mwisho na kuwapindua wakali hao wa Merseyside na kubeba 'ndoo'.
"Sikushangazwa," alikiri Pellegrini.
"Nilikuwa na uhakika pale niliposema kwamba, "Liverpool wanatakiwa kuwa
makini kwasababu wanahitaji kucheza mechi nne zaidi na presha ilizidi
kuongezeka kila baada ya mechi wakiwa kileleni"
Jalamba: Manchester City wakijiandaa na mechi ya jumatatu uwanja wa Etihad dhidi ya Liverpool
Ataweza?" Frank Lampard amesema yuko tayari kucheza dhidi ya Liverpool
Pellegrini anafikiria kuanza na Sergio
Aguero aliyefunga bao katika mchezo wa ufunguzi na kuwapa ushindi wa
mabao 2-0 dhidi ya Newcastle wikiendi iliyopita.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Bosnian,
Edin Dzeko anatarajia kuiongoza safu ya ushambuliaji, lakini nyota mpya
aliyesajiliwa kwa dau la paundi milioni 32, Eliaquim Mangala hayuko tayari kucheza baaada ya kujiunga na timu wiki iliyopita akitokea Porto .
0 comments:
Post a Comment