Mkuu
wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma
Masauni akionesha Kifaa “THERMAL SCANNER” kwa Wafanyakazi wa Kituo cha
Afya cha Uwanja wa ndege wa Zanzibar. Kifaa hicho kitatumika kusaidia
kuwabaini Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia nchini kutoka mataifa mengine.
Mkuu
wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma
Masauni na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Zanzibar wakionesha
baadhi ya Vifaa Vitalavyotumika kuwachunguza Wagonjwa wa EBOLA watakao
ingia nchini kutoka mataifa mengine
Mkuu
wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma
Masauni akionesha matumizi ya Kifaa cha “THERMAL SCANNER” kwa
Wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Uwanja wa ndege wa Zanzibar. Kifaa
hicho kitatumika kusaidia kuwabaini Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia
nchini kutoka mataifa mengine.
Wizara ya Afya Zanzibar imekabidhi
kifaa cha THERMAL SCANNER kwa ajili ya kuchunguza Wagonjwa wa EBOLA
watakao ingia nchini kutoka mataifa mengine.
Kifaa hicho kilichowekwa katika
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume kitatumika kwa ajili
ya kuwachunguza zaidi Wageni ambao watatoka katika nchi zilizoathiriwa
na Ugonjwa wa Ebola.
Akikabidhi kifaa hicho Mkuu wa
kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma Masauni
amesema THEMO SKAN kitasaidia katika kuwabaini watu ambao wameathirika
au kuwa na dalili za Ungojwa wa Ebola na kuchukuliwa hatua zaidi.
Dkt Salma amesema iwapo mgonjwa
atabainika hatua zaidi zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kupelekwa katika
kituo cha Afya cha Chumbuni ambacho kimetayarishwa kwa ajili hiyo.
Aidha Dkt Salma amefahamisha kuwa
Kituo cha Afya cha Chumbuni kimetengwa kama eneo litakalotumika kwa
ajili ya Matibabu kwa mgonjwa atakayebainika kuambukizwa Ugonjwa wa
Ebola nchini.
Amesema Wizara ya Afya katika
kukabiliana na Ugonjwa huo wa kuambukiza imekuwa ikifanya Jitihada
mbalimbali za kutoa elimu na njia mbali mbali za kinga kabla ya Zanzibar
kuathirika na Ebola.
Amesema licha ya Vifaa hivyo
vilivyotolewa Vifaa vingine vitakuja wiki inayokuja ili viendelee
kutumika katika maeneo ya Bandarini na Viwanja vya ndege Unguja na Pemba
Dkt. Salma amesema Ugonjwa huo
haujaingia nchini bali Serikali inajiandaa na juhudi zake za kukabiliana
na Ugonjwa huo ili usiweze kuingia na kuathiri Zanzibar.
Na Faki Mjaka Maelezo Zanzibar 28/08/2014
0 comments:
Post a Comment