Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela
--------------------------------------------------
Jeshi
la polisi mkoani ruvuma liwashikilia askari wake wawili kwa kosa la
kumjeruhi dereva pikipiki wenye umri wa mika (22) aliyetambulika kwa
jina la salgo ndunguru mkazi wa mtaa wa ruvuma manispaa ya songea mkoani
ruvuma .
Kamanda
wa jeshi hilo la polisi mkoa wa Ruvuma mihayo msikhela akizungumza na
mtandao huu amewataja askari ambao wanaoshikiliwa jeshi hilo kuwa ni
askari no.G5075 PC WAZAIRI na askari no G9800 PC AYOUB wakiwa katika
doria na pikipiki ya polisi yenye namba za usajiri CR aina ya YAMAHA
CC.250 katika maeneo ya mkombezi kata ya mfaranyaki manispaa ya songea
walimjeruhi SALGO S/O NDUNGURU kwa risasi mkono wa kushoto na paja la
mguu wa kushoto baada ya kumkamatwa kwa kosa la usalama barabarani.
Ameendelezea
kueleza kuwa baada ya Agreyi ambaye ni dreva wa pikipiki yenye namba za
usajiri T.757 kukamatwa kwa kosa hili ndipo alipompigia simu kijana
huyo ambaye ni majeruhi na kumjulisha kukamatwa kwake na askari kwani
yeye ndiye mdhamini wa pikipiki hiyo.
Amesema
baada ya kufika kwake eneo hilo ndipo mkusanyiko wa waendesha pikipiki
wanaoujilikana kwa jina maarufu kama bodaboda (YEBO YEBO)ukwa mkubwa na
na kuanza kurushiana na askari hao mawe huku majeruhi huyo akiwa
ameshika mtutu wa bunduki iliyokuwa imebebwa na askari no G 9800 PC
AYUBU na ndipo askari namba G5075PC WAZIRI katika kuinusurusilaha hiyo
isiporwe alimpiga sehemu mbili ambazo ni kiganja cha mkono wa kushoto na
paja la mguu wa kushoto.
"Upelelezi
wa tukio hilo tayari umekwishaanza ili kubaini chanzo halisi cha tukio
hilo na askari husika tunawashikilia kwa mahojiano zaidi ili tuweze
kuchukua hatua sitahiki.)alisema kamanada
Aidha
amesema mpka hivi sasa majeruhi huyo amelazwa katika hosipitali ya
rufaa ya mkoa wa ruvuma ili kupatiwa huduma ya matibu huku hali yake
ikiwa inaendelea vizuri.
0 comments:
Post a Comment