Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ametabiri
hatima ya maisha yake hapa duniani ikiwa ni mwaka mmoja tangu aachiwe
kiti hicho na Papa Benedict XVI aliyeng’atuka kutokana na matatizo ya
kiafya.
Akiongea na waandishi wa habari kwenye ndege wakati akirejea Vatican
kutoka ziarani nchini Korea Kusini, Papa Francis amesema kuwa suala la
kuendelea kuishi ni neema ya Mungu na kwamba atafariki baada ya miaka
miwili au mitatatu.
“Suala hili naliona kama neema tu ya Mungu kwa watu wake. Najaribu
kutafakari kuhusu dhambi zangu na makosa yangu, siwezi kujivuna. Najua
kwa sababu hali hii itadumu kwa muda mchache. Miaka miwili au mitatu
nitakuwa nimeondoka na kwenda nyumbani kwa baba.” Amesema Papa Francis.
Ingawa Papa Francis mwenye umri wa miaka 77 hajawahi kuzungumza
hadharani kuhusu suala la afya yake, lakini baadhi ya vyanzo vya habari
kutoka Vatican vimeeleza kuwa amekuwa akiwaambia watu wake wa karibu
kuhusu siku zake chache zilizosailia dunia.
Wachambuzi wa masuala ya kiimani wameeleza kuwa huenda Papa Francis ana tatizo la kiafya ambalo hakuliweka wazi.
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment