Saturday, 23 August 2014

SAMATTA WATUA KINSHASA TAYARI KWA PAMBANO NA AS VITA KESHO

 

Mshambuliaji Mbwana Samatta wa TP Mazembe ya Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya kuwasili na timu yake hiyo mjini Kinshasa, wakitokea Ndola, Zambia walipokuwa wameweka kambi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya DRC dhidi ya mahasimu wao wakubwa, AS Vita ya mjini humo, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Tata Raphael, Kinshasa kesho jioni. Mazembe iliweka kambi ya wiki Ndola kwa ajili ya mchezo huo. Mbali na mchezo wa kesho, timu hizo zitakutana tena Oktoba 22 katika mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika kuamua timu ya kuongoza Kundi A.

0 comments: