Afisa uhamasishaji wa nyanda za juu kusini Charton Meena |
KATIKA kukabiliana na changamoto ya uchangiaji damu Kitengo
cha damu salama hospitali ya meta mkoani mbeya kimewataka wananchi mkoani hapa
kujitokeza kwa wingi katika suala la uchangia damu ili kuweza kuwasaidia watu
mbalimbali.
Meena amesema kuwa uhitaji wa damu unahitajika kwa wingi
kutokana na matukio mbalimbali ya ajali na magonjwa ya akina mama na watoto ambapo
husababisha mahitaji ya damu kwa wingi.
Aidha Meena amesema kuwa njia zinazo tumika kuwafikia wananchi
ili kuhamasisha kuchangia damu ni kutumia
vipeperushi, mitandao ya kijamii ,vyombo vya habari.
Hata hivyo Meena ameongeza kuwa zipo changamoto mbalimbali
katika suala la kuchangia damu ambapo amesema changamoto hizo ni uwoga
wawananchi,mila potofu pamoja na imani za kinidi.
muonekano wa hospital ya wazazi meta ambapo ndio makao makuu ya damu salaama nyanda za juu kusini |
makao makuu ya damu salaama nyanda za juu kusini |
Charton Meena |
0 comments:
Post a Comment