Waziri
wa Nishati na Migodi wa Burundi Mhe. Côme Manirakiza (aliyeinua mkono),
akiomba kupewa ufafanuzi kuhusu sekta ya madini hapa nchini, baada ya
uwasilishwaji mada zilizohusu sekta za nishati na madini za Tanzania.
Waziri Manirakiza na Ujumbe wake walitembelea Makao Makuu ya Wizara ya
Nishati na Madini – Dar es Salaam, Agosti 26, 2014 kwa lengo la
kujifunza namna sekta husika zinavyofanya kazi. Wengine pichani ni
Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini – Tanzania (kushoto) na Ujumbe
ulioongozana na Waziri (Kulia).
Kaimu
Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje akiwasilisha mada kuhusu Sekta
ya Madini – Tanzania kwa Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe.
Côme Manirakiza (wa kwanza kulia) na Ujumbe wake (Kulia kwake) waliofika
Makao Makuu ya Wizara – Dar es Salaam, Agosti 26, 2014 kujifunza namna
Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi. Upande wa kushoto ni
Wataalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake.
Na Veronica Simba
Waziri wa Nishati na Migodi wa
Burundi, Mhe. Côme Manirakiza na Ujumbe wake wako katika ziara ya siku
tano (24 – 28 Agosti, 2014) hapa nchini kwa lengo la kujifunza namna
Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi.
Katika ziara yake, Waziri
Manirakiza ametembelea Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini – Dar
es Salaam na kukutana na Wataalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi
zilizo chini yake wakiongozwa na Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally
Samaje.
Wakiwa Wizarani, Waziri na Ujumbe
wake walipata fursa ya kusikiliza mada zinazohusu Sekta za Nishati na
Madini zilizowasilishwa na Wataalamu wa Wizara.
Ujumbe huo pia umepata nafasi
kutembelea Taasisi na Mashirika mbalimbali yaliyo chini ya Wizara na
yale yenye uhusiano na Wizara ikiwemo Mpango wa Uwazi na Uwajibikaji
katika Tasnia ya Uziduaji Tanzania (Tanzania Extractive Industry
Transparency Initiative – TEITI), Mradi wa Usimamizi Endelevu wa
Rasimali Madini (SMMRP) na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).
0 comments:
Post a Comment