Waziri wa habari wa Liberia amekiri kuwa jinsi ugonjwa wa ebola unavotapakaa umezidi nguvu za huduma za afya za nchi.
Lewis Brown ameiambia BBC mfumo wa afya umefikia kikomo lakini alikanusha tuhuma kuwa serikali ilichelewa kuchukua hatua, akisema kuwa wakuu wanafanya wawezalo kukabiliana na janga wasilopata kukumbana nalo.
Alisema wananchi wengi bado hawakukubali ukweli halisi kuhusu ebola.
Shirika la msaada wa matibabu la kimataifa, MSF (Medicins Sans Frontiers), limesema kwamba makisio ya wizara ya afya ya Liberia ni madogo ikilinganishwa na ukweli ulioko nchini.
Hapo Jumamosi polisi wa kupambana na fujo walivunja maandamano dhidi ya serikali kwa namna ilivoshughulikia hali hiyo.
Inakisiwa kuwa ebola imeuwa watu karibu 1,000 nchini Liberia, Guinea,Sierra Leone na Nigeria.
0 comments:
Post a Comment