WATU WAWILI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWA TUHUMA ZA MAUAJI.
· MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA JIWE KICHWANI.
WATU WAWILI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWA TUHUMA ZA MAUAJI.
WATU WAWILI
WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA MAKOJA PIMA (50) NA MARITHA MAZENGO (45)
WOTE WAKAZI WA KILOMBERO WALIUAWA KWA KUPIGWA NA GONGO KICHWANI NA
MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. TUKIO HILO LILITOKEA MAJIRA YA SAA 03:00HRS
USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KILOMBERO WILAYANI CHUNYA
BAADA YA WATU HAO KUWAVIZIA WAKIWA WAMELALA NA KISHA KUWAPIGA NA GONGO
KICHWANI HALI ILIYOPELEKEA KUPOTEZA MAISHA. UCHUNGUZI WA AWALI
UNAONYESHA CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA.
WATUHUMIWA WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWA
MAHOJIANO ZAIDI AMBAO NI MWANYI LEPONA (46) MKAZI WA KILOMBERO NA MKWAJU
SIMON (25) MKAZI WA MACHINJIONI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUAMINI IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA
MAKUBWA KWA JAMII. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA
MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA JIWE KICHWANI.
MTU MMOJA
ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA DESI OMARI (39) MKAZI WA MTAA WA MAPOROMOKO
ALIUAWA KWA KUPIGWA JIWE KICHWANI NA BISODI MWANJISI. TUKIO HILO
LILITOKEA MAJIRA YA SAA 21:00HRS USIKU HUKO KATIKA MTAA WA MAPOROMOKO
WILAYA YA MOMBA BAADA YA MAREHEMU KUMFUMANIA MTUHUMIWA AKIWA NA MKE WAKE
AITWAYE FATUMA MSONGOLE (32). MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO
NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. FATUMA MSONGOLE ANASHIKILIWA NA
JESHI LA POLISI KWA MAHOJIANO ZAIDI KUTOKA NA TUKIO HILO. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA
WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA
ICHUKUE MKONDO WAKE.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment