Sunday, 25 October 2015

Wagombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi za CCM na CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, na DK Ali mohammed shein tayari wameishapiga Kura...


Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, tayari amepiga kura yake kwenye Kituo cha Mtoni, Chumba Na. 13.

Tofauti  na  ilivyokuwa  kwa  mgombea  Urais  wa  CCM, Dr Shein, Maalim yeye  amedai kwamba kura yake ni siri yake lakini ana matumaini ya ushindi wa asilimia 72.

 Na Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohammed Shein Ameshapiga Kura


Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Ali Mohammed Shein, tayari ameshapiga kura yake kwenye Kituo cha Skuli ya Bungi kusini mwa kisiwa cha Unguja, majira ya saa moja asubuhi 
Shein  amewaambia  waandishi  wa  habari   kuwa amejipigia kura mwenyewe na ana matumaini makubwa yakushinda 
 

0 comments: