Saturday, 24 October 2015

Hii ndyo taarifa sahii kuhusu Dr Mary Nagu kukamatwa na Masanduku 10 ya Kura yaliyopigwa Tayari

 


Taarifa ya awali:

Wakuu kwa habari za hivi punde kutoka Hanang ni kuwa Dr Mary Nagu amekamatwa na maboksi kumi ya kura yakiwa yashapigiwa kura tayari huko Hanang. Sasa hivi amekamatwa yupo Polisi,taarifa zaidi zinakuja.

 
TAARIFA SAHIHI:

JamiiForums imemtafuta RPC wa Mkoa wa Manyara, Christropher Fuime na kufahamishwa kuwa taarifa hizi ni za uwongo na zenye malengo ya kisiasa.

Masanduku yote ya kupigia kura yapo mikononi mwa mamlaka husika na hakuna mtu yeyote aliyekamatwa na sanduku la kura wala wao kama Polisi hawana taarifa toka jimbo lolote mkoani humo kuhusiana na hili.

Mamlaka zimeanza kumtafuta aliyeanzisha uvumi huu!

0 comments: