HOME »
» Mkurugenzi wa Uchaguzi akizungumzia kuahirishwa kwa Uchaguzi Kata ya Saranga na Jimbo la Kwela Sumbawanga
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha uchaguzi katika Kata
ya Saranga iliyoko Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kutokana na kuharibiwa
kwa vifaa vya upigaji Kura ambavyo walikabidhiwa wasimamizi wasaidizi wa vituo
wasio waaminifu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kailima
Ramadhani aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake kuwa vituo 14 katika
eneo la Stop over Kimara,vituo 8 katika eneo la IDP royal na kituo kimoja
katika eneo la Mavurunza viliathirika na uharibifu huo wa vifaa hivyo
havitaweza kupiga Kura. Aliongeza kuwa kuna vituo 8 katika kata ya Msigani
ambavyo pia vililazimika kuahirisha uchaguzi kutokana na kuharibiwa kwa
masanduku ya kupigia Kura kulikosababishwa na vurugu.
Aidha katika Kata ya
Milepa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga vituo 15 wapiga Kura walikataa
kuendelea na Uchaguzi kutokana na vifaa kuchomwa moto zikiwemo karatasi za
kupigia Kura pamoja na Masanduku ya Kura. Kwa minajili hiyo wapiga Kura katika
maeneo hayo yote watalazimika Kupiga Kura kesho kumchagua Rais na baadae Tume
itatoa maelekezo juu ya Uchaguzi wa Bunge Jimbo la Kwela na Udiwani katika kata
ya Saranga.
0 comments:
Post a Comment