Gari lilokodiwa na tume ya uchaguzi ya Wilaya ya Arumeru Mashariki limezua utata baada ya kukutwa na kiasi cha fedha zaidi ya Sh 6 milioni.
Akizungumzia sakata hilo, Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi, kata ya Imbaseny , Jefason Mwangura ,amekiri kubeba fedha hizo kwenye gari hilo mali ya Enong’oto na kudai kuwa zilikuwa ni za malipo ya wasaidizi wa vituoni kwa ajili ya kujikimu.
Alisema pia pesa hizo kwa utaratibu ilikuwa ni kulipa wasaidizi vituoni ili iweze kuwasaidia kujikimu wakiwa vituoni hapo .
Hata hivyo , Mwangura alisema Mwenyekiti wa Chadema, kata ya Imbaseny baada ya kukamata fedha hizo alikimbia nazo kusikofahamika.
“Mimi nashangaa hela zimechukuliwa na aliyechukua amekimbia nazo ,” kama ilikuwa si halali wangezishika wasubiri polisi ,”alisema Jefason
Mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,(chadema) Joshua Nasari alizungumzia tukio hilo na kusema ni kosa kisheria kuzunguka na fedha hizo kwani kisheria ilipaswa zilipwe kabla au baada ya uchaguzi.
0 comments:
Post a Comment