Monday, 26 October 2015

Lowassa Kaongea na Vyombo vya Habari Mchana Huu...



Nimewaita kueleza masikitiko yetu mawili haswa katika upande wa jeshi la Polisi. Tuna vijana wetu wanaofanya kazi za IT kwa kujitolea maeneo ya kinondoni na kijitonyama jumla ya vituo vitatu.

Hawa vijana wanafanya uzalendo,kushiriki katika uchaguzi wa nchi yao,na kujenga historia moya ya nchi yao,tendo la kuwakamata si la haki kabisa

Wamewavamia na kuwakamata kwa kosa la human trafficking ambalo ni kosa kubwa na halifanani na kazi wanazofanya.
 
Nimeona taarifa zao za matokeo ya kura wameanza kuonyesha watu taratibu zinazompendelea Magufuli.

Ningependa kuwashauri tume watoe matokeo yote kwa pamoja, Sio kufanya kama hivi wanavyotoa kidogo kidogo yanayoongelea upande wa pili kushinda,wanafanya maandalizi ya kisaikolojia (psychological preparedness) kudhoofisha morali ya wafuasi wa UKAWA ambayo si haki

Swali;
Give us your view So far on the tallying

Jibu;
So far so good. Ila napenda kutoa pongezi kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi kupia kura,Wamekua watulivu na kuheshimu sheria na kanuni.

Swali;
You said the main tallying station has been raided, Do you have an alternative?

Jibu;
We have no alternative, we have been handicapped
They have been so unfair .I wish i could charge them in ICC

Swali;
Chadema ina mpango gani kuwatoa hao waliokamatwa?

Jibu;
Jumla yao walikua 191 wanajumlisha kura, Sisi hatuna hatua stahiki zaidi ya kuongea na nyie waandishi wa habari mpeleke taarifa hizi duniani, kwamba huu ni uonevu mkubwa.

0 comments: