Jose Mourinho amemponda Marc Wilmots kuhusu madai yake kwamba Eden Hazard ataondoka Chelsea na kuhamia Real Madrid
Msimu uliopita Hazard, ambae ni Mchezaji wa Kimataifa wa Belgium, alitunukiwa Tuzo ya PFA pamoja na ile ya Wanahabari ya kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka huko England lakini Msimu huu uchezaji wake umeporomoka.
Wiki iliyopita Mourinho alimpiga Benchi Hazard wakati Chelsea inaifunga Aston Villa 2-0 kwenye Ligi kwa madai kuwa anataka kuzuia Timu yake isiruhusu Mabao.
Magazeti kadhaa huko England yalimnukuu Marc Wilmots, ambae ni Kocha wa Timu ya Taifa ya Belgium, akisema Hazard, mwenye Miaka 24, anapaswa kuhamia Real Madrid ilia pate uhuru zaidi wa kucheza na pia kukwepa sulubu nzito ya Soka la England.
Maneno hayo yamemkasirisha Mourinho ambae amesema: "Kocha wa Timu ya Taifa ni wa Taifa. Hazard akiwa Timu ya Taifa mimi sisemi lolote. Lakini Watu wengine hawana maadili na wanazungumzia Wachezaji wakiwa Klabuni kwao!”
Alipoulizwa kama Hazard atacheza hii Leo dhidi ya West Ham, Mourinho alijibu: “Sijui. Kuna Watu wengi wanatoa maoni yao kuhusu uchezaji wa Hazard Msimu huu. Mimi sipendi kuzungumzia Mtu binafsi.”
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 24
1700 Aston Villa v Swansea
1700 Leicester v Crystal Palace
1700 Norwich v West Brom
1700 Stoke v Watford
1700 West Ham v Chelsea
1930 Arsenal v Everton
Jumapili Oktoba 25
1500 Sunderland v Newcastle
1705 Bournemouth v Tottenham
1705 Man United v Man City
1915 Liverpool v Southampton
0 comments:
Post a Comment