Umoja wa katiba ya wanachi ukawa umehitimisha kampeni zake katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam ambapo mwenyekiti wa taifa wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema Mh.Freeman Mbowe amesema ushindi ni lazima.
Akihutubia maelfu ya wanachama wa chama hicho Mh.Mbowe amesema ushindi ni lazima na hivyo amewataka wananchi kushangilia ushindi.
Naye mgombea urais kwa tiketi ya chadema Mh.Edward Lowassa amesema safari ya kampeni ilikuwa ngumu na yenye changamoto nyingi lakini jambo jema zimeisha salama kikubwa watu wajitokeza kwenda kupiga kura.
Akitoa salamu zake mgombea urais visiwani Zanzibar kwa tiketi cha chama cha wananchi CUF Mh.Seif Sharif Hamad amesema wazanzibar wamejipanga vyema na wamesema watamchagua Lowassa naye mgombea mwenza Mh.Juma Duni Haji amewataka wananchi kulinda kura zao.
Akitoa salamau zake mzee Kingunge Ngombare Mwiru amesema CCM imechoka na kwa upande wake Mh.James Mbati mwenyekiti mwen za UKAWA amesema ni bora CCM ikubali kuachia madaraka kwa amani bila ya vurugu.
0 comments:
Post a Comment