Saturday, 24 October 2015

KINGUNGE : WATANZANIA SASA KUMEKUCHA MAMBO YANAENDA

Mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombare -Mwiru akiwa jukwaani
Mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombare -Mwiru akiwa jukwaani


“KUMEKUCHA, mambo yanaenda mpoto mpoto, wananchi wamechoka, wanataka mabadiliko na maisha bora ambayo Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameshindwa kuyatekeleza,” ndivyo anavyosema aliyekuwa kada wa CCM, Kingunge Ngombare-Mwiru. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).
Akihutubia wananchi leo kwenye mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wa kufunga kampeni za mgombea urais wa chama hicho anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, Kingunge amesema Watanzania wameichoka CCM.
Mkutano huo ulihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Ukawa, miongoni mwao ni mgombea mwenza wa chama hicho, Juma Duni Haji; mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe, wagombea ubunge wa Dar es Salaam kupitia Ukawa pamoja na mgombea urais Zanzibar kupitia Chama Cha wananchi Zanzibar (CUF), Seif Sharif Hammad.
Katika hotuba yake Kingunge amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuiondoa madarakani kwa kile alichosema “CCM imeishiwa pumzi hivyo haiwezi tena kuongoza”
“Rais Jakaya Kikwete aliwaahidi wananchi maisha bora kwa kila mtanzania kabla ya kuingia madarakani lakini baada ya kuingia wananchi wamekiona cha moto. Tatizo sio sera tu hata viongozi wanaoingia ni wabovu, ndio maana Lowassa alipotaka urais walimnyima kwa kuwa waliona atawaumbua.
“Nimekaa CCM miaka 61 lakini siku izi imeharibika, sio ile ya zamani. Niliona haifai kundelea kubaki huko ndio maana nikatoka, nimewaacha wanalia huko nyuma hawajielewi na ndio maana wanafanya mambo ya ajabu kwa kuwa wamechanganyikiwa,” amesema Kingunge.
Aidha katika hutuba yake pia amemtaka Rais Kikwete kuachia madaraka kwa amani kama ambavyo aliachiwa na marais waliopita.
“Ukiachia nchi hii kumkabidhi Lowassa kwa amani hata nchi itakuheshimu na hata familia yako itakuheshimu. Na endapo ukisababisha machafuko nchini basi nchi hii haitakusamehe.
“Watanzania wanataka mabadiliko kwa kuwa wameshoka kuonewa. Hawako tayari kuongozwa na nyampala wa barabarani, wanamtaka rais mwadilifu mwenye kujua kazi yake akiwa kiongozi,” amesema Kingunge.
Mbali na Kingunge pia viongozi wngine waliopata kuhutubia katika mkutano huo wamendelea kuwasisitiza wananchi kubaki eneo la kituo baada ya kupiga kura ili kuzilinda kwani CCM wanambinu chafu za kuiba kura.
Kiongozi mmoja wapo aliyepata kuhutubia mkutano huo, Mbowe amesema, Wananchi wanatakiwa kulinda kura zao kwani Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inafanya mipango ya kuiba kura kwa kushirikiana na CCM, hivyo haiaminiki.
“Kesho ni siku ya kuamua maisha yetu tuyaweke vizuri, Mungu atakwenda kujibu maombi yetu.Kwa namna tunavyoona ushindi ni lazma na tutazijua kura zetu kabla NEC haijatangaza.
Naye mwenyekiti mwenza wa Ukawa Francis Mbatia amemtaka Kikwete kuacha mara moja mbinu za kutaka kusababisha fujo ili asitoke madarakani.” Naapa Kikwete uchaguzi ukiisha usipotoka tutakutoa hata kwa mlango wa nyuma wananchi hawatakubali kwani wameshachoka”. 

0 comments: