Monday, 26 October 2015

MATOKEO YA AWALI: Dk Magufuli anaongoza majimbo tisa, Lowassa manne



Dk John Pombe Magufuli
Dar es salaam.Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jioni hii imeendelea kutoa matokeo ya awali ya urais katika majimbo 13 ambapo mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli anaongoza kwa majimbo tisa wakati Mgombea wa Chadema, Edward Lowassa anaongoza majimbo manne.

Matokeo hayo yametangazwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Damian Lubuva kwa awamu mbili, ambapo asubuhi  mwenyekiti huyo alitangaza majimbo matatu ambayo ni  Paje, Makunduchi na Lulindi ambayo yote Dk Magufuli ameongoza.
Majira ya alasiri , Jaji Lubuva alitangaza majimbo mengine 10 ambapo kati ya hayo majimbo sita yalionyesha Dk.Magufuli anaongoza huku majimbo manne yakionyesha Lowassa anaongoza.
Majimbo hayo ni pamoja na Jimbo la Ndanda (Dk Magufuli), Nsimbo (Dk Magufuli), Kiwani (Lowassa), Chambani (Lowassa), Mtambile (Lowassa), Mkoani (Lowassa), Kibaha Mjini (Dk Magufuli), Bumbuli (DK Magufuli), Donge (DK Magufuli) na Jimbo la Kiwengwa (Dk Magufuli)
Jaji Lubuva amesema kuwa matokeo ya majimbo mengine ambayo yatakuwa tayari yatatolewa leo saa mbili usiku.
     

0 comments: