Sunday, 25 October 2015

MOURINHO, CHELSEA MAJI SHINGONI, WABONDWA NA KADI NYEKUNDU JUU!

         LIGI KUU ENGLAND

RATIBA/MATOKEO:
**Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 24
Aston Villa 1 Swansea 2                  
Leicester 1 Crystal Palace 0      
Norwich 0 West Brom 1           
Stoke 0 Watford 2          
West Ham 2 Chelsea 1    
1930 Arsenal v Everton
          
West Ham 2 Chelsea 1
MOURINHO-JUKWAANIChelsea Leo wamepokea kipigo chao cha 5 katika Mechi zao 10 za Ligi Kuu England Msimu huu na kushuhudiAa Kiungo wao Nemanja Matic na Meneja wao Jose Mourinho wakitolewa nje ya Uwanja.
Wakicheza Ugenini huko Upton Park, Chelsea walifungwa Bao 2-1 na West Ham na kujikuta wakizidi kudidimia mkiani mwa msimamo wa Ligi.
West Ham walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 17 kupitia Mauro Zarate lakini kabla ya Haftaimu Kiungo wao Nemanja Matic alipewa Kadi za Njano 2 ndani ya Dakika 9 na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Wakati wa Haftaimu, Jose Mourinho nae alipewa Kadi Nyekundu kwa kumzonga Refa Jon Moss.
Chelsea walisawazisha Dakika ya 56 kwa Bao la Kichwa la Gary Cahill kufuatia kona lakini Dakika ya 79 Andy Caroll aliipa West Ham ushindi kwa Bao la Kichwa.
VIKOSI:
West Ham: Adrian, Jenkinson, Collins, Tomkins, Cresswell, Noble, Kouyate, Lanzini, Payet, Zarate, Sakho.
Akiba: Randolph, Carroll, Valencia, Obiang, Ogbonna, Jelavic, Antonio.
Chelsea: Begovic, Zouma, Cahill, Terry, Azpilicueta, Matic, Ramires, Willian, Fabregas, Hazard, Costa.
Akiba: Baba, Oscar, Falcao, Mikel, Traore, Amelia, Loftus-Cheek.
REFA: Jon Moss
Norwich 0 West Brom 1
Bao la Dakika ya 46 la Salomon Rondon limewapa ushindi wa Bao 1-0 West Brom waliokuwa Ugenini kucheza na Norwich.
VIKOSI:
Norwich: Ruddy, Martin, Bennett, Bassong, Brady, Redmond, Tettey, Howson, Jarvis, Hoolahan, Mbokani.
Akiba: Whittaker, Grabban, Jerome, Rudd, Dorrans, Olsson, O’Neil.
West Brom: Myhill, Dawson, McAuley, Evans, Brunt, Sessegnon, Fletcher, Yacob, McClean, Rondon, Berahino.
Akiba: Olsson, Chester, Gardner, Anichebe, Lambert, McManaman, Lindegaard.
REFA: Kevin Friend
Leicester City 1 Crystal Palace 0
Leicester wameendeleza mwanzo wao mzuri kwenye Ligi kwa kuifunga Crystal Palace Bao 1-0.
Bao lao la ushindi lilifungwa Dakika ya 59 na Jamie Vardy.
VIKOSI:
Leicester: Schmeichel, Simpson, Morgan, Huth, Fuchs, Albrighton, Drinkwater, Kante, Schlupp, Mahrez, Vardy.
Akiba: De Laet, King, Kramaric, Okazaki, Dyer, Schwarzer, Inler.
Crystal Palace: Hennessey, Kelly, Hangeland, Dann, Mariappa, Cabaye, McArthur, Sako, Puncheon, Bolasie, Campbell.
Akiba: Speroni, Bamford, Zaha, Jedinak, Mutch, Delaney, Ledley.
REFA: Mike Dean
Stoke 0 Watford 2
Stoke City wakiwa kwa Leo wamefungwa 2-0 na Watford kwa Bao za Troy Deeney na Almen Abdi.
VIKOSI:
Stoke: Butland, Johnson, Cameron, Wollscheid, Pieters, Adam, Whelan, Shaqiri, Krkic, Arnautovic, Joselu.
Akiba: Ireland, Wilson, Afellay, van Ginkel, Walters, Given, Crouch.
Watford: Gomes, Nyom, Britos, Cathcart, Ake, Watson, Capoue, Abdi, Deeney, Anya, Ighalo.
Akiba: Prodl, Behrami, Paredes, Guedioura, Ibarbo, Diamanti, Arlauskis.
REFA: Martin Atkinson
Aston Villa 1 Swansea City 2
Presha kwa Meneja wa Aston Villa inazidi kuendelea baada ya kuchapwa 2-1 wakiwa kwao na Swansea City.
Villa walitangulia kufunga kwa Bao la Jordan Ayew katika Dakika ya 62 lakini Dakika ya 68 Gylfi Sigurdsson akaisawazishia Swansea kwa Frikiki na Andre Ayew, Kaka wa Jordan Ayew, akaipa Swansea ushindi kwa Bao la Dakika ya 87.
VIKOSI:
Aston Villa: Guzan, Hutton, Richards, Lescott, Richardson, Bacuna, Gana, Ayew, Grealish, Agbonlahor, Gestede.
Akiba: Westwood, Traore, Amavi, Sanchez, Gil, Bunn, Crespo.
Swansea: Fabianski, Naughton, Fernandez, Williams, Taylor, Ki, Shelvey, Ayew, Sigurdsson, Montero, Gomis.
Akiba: Britton, Nordfeldt, Eder, Rangel, Cork, Bartley, Barrow.
REFA: Neil Swarbrick
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumapili Oktoba 25
1500 Sunderland v Newcastle                  
1705 Bournemouth v Tottenham              
1705 Man United v Man City           
1915 Liverpool v Southampton

0 comments: