Saturday, 24 October 2015

MAKUBWA YA UCHAGUZI HUU: MADEREVA WAMEJIPA SIKUKUU...!

0_b6f72.jpg

Ndugu zangu,
Kwenye taarifa ya habari usiku huu nimemsikia kiongozi wa chama cha madereva wa mabasi akitangaza kuwa kesho madereva wanapumzika kuendesha mabasi ili wapige kura kutimiza haki yao ya kikatiba.
Nimetafakari jambo hilo na kuhisi harufu ya siasa ndani yake.
Nimeshuhudia chaguzi nyingi nchi hii. Ni mara ya kwanza leo kusikia kuwa siku ya uchaguzi madereva wa mabasi wanapumzika.
Duniani hapa kazi nyingine ni lazima wawepo watu wa kuzifanya, kila siku. Hazina sikukuu.
Dr. Remmy alipata kuimba wimbo kuwasifu madereva na kusema;
" Dereva hana sikukuu".
Tutafanyaje siku ile na manesi wote nao wakidai kupumzika wapige kura kutimiza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura. Na madaktari? Na manahodha wa meli...
Nilidhani, kuwa chama cha madereva wa mabasi kingejipangana mapema kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi ili siku kama ya kesho madereva wote wapewe kipaumbele kupiga kura mapema na kuendelea na kazi yao ya kusafirisha abiria.
Vinginevyo, utamaduni huu ni wa hatari kuundekeza.
Imeandikwa na Maggid.mjengwa

0 comments: