Saturday, 24 October 2015

Mwigulu Nchemba: Siasa si Uadui, Acheni Kuumizana...Kuna Maisha Baada ya Uchaguzi


Mbeya. 
Mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM, Mwigulu Nchemba amewataka wakazi wa Mbeya kuacha chuki kwa sababu za kisiasa kwani hata viongozi wa CCM na Chadema ni marafiki hawana uadui.

Akizungumza juzi kwenye viwanja vya Uyole na Nzovwe jijini hapa, Nchemba alisema alisikitishwa na taarifa za kuuawa kwa wana CCM wawili katika Mji Mdogo wa Tunduma wakati wa kampeni za Chadema.

“Nimesikitishwa na hatua hii mliyofikia, nimesikia kuna watu wawili Tunduma wameuana kwa sababu za kisiasa,” alisema Nchemba.

Alisema ubishi wa kisiasa unapaswa kulenga katika kuimarisha maendeleo ya watu na Taifa, lakini udugu lazima ubaki palepale.

Aliwasihi wakazi hao kutokubali kuumizana kwa sababu ya siasa kwani haitawasaidia.

Mgombea udiwani wa Kata ya Nzovwe, Mlaga alisema endapo wananchi watamchagua atahakikisha kivuko cha Mto Swaya kinatengenezwa.
Source:Mwananchi 

0 comments: