Saturday, 24 October 2015

RPC aonya makundi yanayotaka kufanya vurugu Arusha

Kamanda Mkuu wa polisi mkoa Arusha, Liberatus Sabas amesema jeshi hilo limebaini uwepo wa vikundi vilivyojipanga kufanya vurugu na kuvionya kuacha mara moja.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ,amesema mpaka sasa wameweza kubaini zaidi ya watu 100 wakiwa ni vijana ambao wamesambazwa Arusha mjini pamoja na wilaya ya Arumeru kwaajili ya kufanya vurugu wakati wa uchaguzi .

Amesema jeshi la polisi limejipanga kukabiliana na uhalifu au vurugu zozote zitakazotokea katika kipindi cha uchaguzi kwa kuwa tayari wamepokea tetesi za kuwepo kwa makundi hayo.

“Natoa onyo kwa hayo makundi kuwa kama wanataka usalama waache mara moja zoezi hilo, kwa kuwa hawatakuwa salama ,”amesema Liberatus .

Kamanda huyo amewataka wakazi wa Arusha kuzipuuzia dhana potofu kuwa polisi wapo kwa ajili ya kupiga wanachi na  kusema kuwa sheria itachukua mkondo wake kwa watakaofanya vurugu.

“ Kazi ya polisi si kupiga watu ,kazi ya polisi ni kulinda, sisi tunasema ukipiga kura na uende kwako kama sheria inavyosema ,hakuna kukaa mita 200 ,300 hata 500 ,wote waende nyumbani ,” amesema.

0 comments: