7.14am:Katika kituo cha Dodoma foleni ndefu imeshuhudiwa ,ni kituo kilichopo katikati ya mji.Baadhi ya wapiga kura waliofika kituoni humo na kupiga kura wanasema hakuna tatizo lolote walilopata.
7.13am:Katika kituo cha kinondondoni tayari watu wameanza kupiga kura bila matatizo yoyote.Sheria ya mita 200 inaonekana kuanza kuheshimiwa kwani watu wanapiga kura na kuondoka vituoni
7.05am:Mtafarufuku umetokeo katika kituo cha masaki baada ya maafisa wa uchaguzi kutoka nje ya vituo vya kupiga kura na kuwaelezea raia kupanga mistari mitatu inayowapendelea wanawake,na wazee.Wengi wa wale waliofika mapema wamepinga hatua hiyo wakidai kwamba ni haki yao kupiga kura wa kwanza.
7.00am:Ni saa moja kamili saa za Afrika mashariki na wakati muhimu kwa taifa la Tanzania ambapo shughuli ya upigaji kura inaanza rasmi
6.30am:Waangalizi wa kimataifa tayari wamefika katika vituo vya kupigia kura katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania ili kushuhudia matukio ya uchaguzi huo.
6.30am: Ili kutaka kufahamu iwapo jina lako liko katika sajili ya uchaguzi wengi wamekuwa wakipiga nambari hizi *152*00#
6.15pm:Usalama umeimarishwa katika kila kituo kulingana na maripota wetu wanaofuatilia matukio mabli mbali ya uchaguzi huu.
6.10am:Maripota wetu wamesambazwa kila maeneo ya taifa hilo ili kuweza kukupatia habari za moja kwa zinazojiri katika maeneo hayo.
6.05pm:Wengi wa watu wamewasili katika vituo hivyo mwendo wa saa kumi na moja asubuhi ili kupata fursa ya kupiga kura hiyo mapema na kuelekea majumbani mwao ili kufuatilia uchaguzi huo katika vyombo vya habari.
6.03am:Tayari maelfu ya watu wamejitokeza katika vituo mbali mbali vya kupigia kura nchini humo ili kushiriki katika zoezi hilo linalotarajiwa kuanza saa moja asubuhi.
6.01am:Ni asubuhi njema na siku muhimu kwa raia wa taifa la Tanzania ambapo raia wanapiga kura kumchagua atakayemrithi rais wa taifa hilo Jakaya Mrisho Kikwete
6.00am:Habari ya asubuhi.
TANZANIA YAAMUA.
19:18pm: Waangalizi wa uchaguzi kutoka eneo la Maziwa Makuu wamesema wamefurahishwa na maandalizi ya uchaguzi.
19:11pm: Zikiwa zimesalia saa machache kabla ya uchaguzi mkuu nchini Tanzania kufanyika, Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo imesema kuwa maandalizi ya shughuli hiyo yamekamilika.
18:00pm: Muda rasmi wa kufanya kampeni umemalizika na sasa kazi ni kusubiri saa moja Oktoba 25 kura zianze kupigwa.
Watanzania wanapiga kura Oktoba 25 kumchagua mrithi wa Rais Jakaya Kikwete anayeondoka madarakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili.
0 comments:
Post a Comment