Saturday, 24 October 2015

breaking news Taarifa kuhusu kuhesabu kura kituoni zaleta mchanganyiko kwa mawakala

Makamanda salaam, kuna taarifa ambayo sio sahihi inasambaa kwa Mawakala na Viongozi wetu kuwa kwenye kituo cha kupiga kura ni kura za Diwani tu zitakazohesabiwa. Taarifa inaeleza kuwa kura za Mbunge na Rais zitahesabiwa kwenye kituo cha majumuisho cha Jimbo. Nimepokea taarifa kutoka Mkoa wa Tanga, Kilimanjaro na Kagera. Taarifa inaonesha kuwa wasimamizi wa vituo ndio waliopewa semina na Wakurugenzi. Tafadhali sambazeni ujumbe kwa viongozi na mawakala wetu kuhakikisha majumuisho yanafanyika kwenye kituo kwa kura za Diwani, Mbunge na Rais. Aidha wahakikishe fomu Na. 21 A, B na C za matokeo (Rais, Mbunge na Diwani) zinajazwa na kuondoka na nakala na kuwasilisha kwa Mratibu wa Kata/Jimbo. Mndeme

chanzo: Chadema in blood pag  na chadema blog

0 comments: