Friday, 23 October 2015

Balozi Seif Atembelea Nyumba za Maendeleo Kisiwani Pemba.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifanya ziara ya kukagua maandalizi ya kazi za usafishaji wa karo zinazohudumia uhifadhi ya Uchafu katika Nyumba za Maendeleo zilizopo Mtaa wa Mtemani Mjini Wete Kisiwani Pemba.
Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Mar Khamis Othman.
 Mkurugenzi wa Baraza la Mji wa Wete Kisiwani Pemba Ndugu Mgeni Othman Juma akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif juu ya hatua zilizochukuliwa katika kufanya usafi wa karo za Nyumba za Maendeleo Mtemani  Mjini Wete.
Balozi Seif akiushauri Uongozi  wa Wizara ya Ardhi na Makaazi kuandaa utaratibu za kuzifanyia ukaguzi Nyumba za Maendeleo ili kukabiliana na changamoto zinazozikabili Nyumba hizo ikiwemo matengenezo ya kila mara.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis OMPR.

Uongozi wa Wizara na Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Kisiwani Pemba kwa kushirikiana na Baraza la Mji wa Wete umeanza matayarisho ya kujiandaa na kazi ya usafishaji wa karo zilizotengwa kuhifadhi uchafu unaotoka katika  Nyumba za Maendeleo zilizopo Mtaa wa Mtemani Mjini Wete Kisiwani Pemba.

Kazi hiyo imeanza kwa hatua ya awali ya uchimbaji  wa mashimo yatakayotumika kufukia mabaki ya uchafu utakaosafishwa kutoka kwenye Karo  Saba  zinazohudumia Nyumba hizo zilizojengwa katika miaka ya sabini.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa Kisiwani Pemba alipata fursa ya kukagua hatua iliyofikiwa ya  kazi hiyo itakayosaidia kuimarisha hali ya usafi pamoja na utunzaji wa  mazingira katika Mtaa huo.

Mkurugenzi wa Baraza la Mji wa Wete Pemba Ndugu Mgeni Othman Juma alimueleza Balozi Seif kwamba Wananchi wa Nyumba za Maendeleo Mtemani Wete wamewahi kujaribu kufanya usafi katika  eneo hilo bila ya kupata mafanikio yoyote.

0 comments: