Wednesday, 21 October 2015

Yanga Vs Toto African na matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu leo October 21

 

Ligi Kuu Tanzania bara imeendelea tena leo Otcober 21 kwa timu 10 kushuka uwanjani kuwania point tatu muhimu, point ambazo zitaisadia kila timu kuwa katika nafasi nzuri katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara kwa msimu wa 2015/2016, msimu ambao kila timu inaonekana kuleta ushindani mkubwa katika kila mechi.
DSC_0036
Kikosi cha Yanga
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania bara Dar Es Salaam Young African, walishuka dimbani katika uwanja wa Taifa Dar Es Salaam kuwakaribisha Toto Africanya Mwanza, huu ukiwa ni mchezo wa saba kwa Yanga wakati kwa upande wa Toto African ambao walikuwa nafasi ya nane katika msimamao wa Ligi Kuu Tanzania bara ni mchezo wao wa nane.
DSC_0033
Kikosi cha Toto African
Dar Es Salaam Young African ambao bado hawajapoteza mchezo hata mmoja kwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu, wameendeleza wimbi la ushindi kwa kuifunga Totot African kwa jumla ya goli 4-1. Magoli ya Yanga yalifungwa na Juma Abdul dakika ya 9, Simon Msuva dakika ya 48 na 90, Amissi Tambwe dakika ya 81 huku goli pekee la Toto African lilifungwa na Miraji Athumani dakika ya 55.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Tanzania bara zilizochezwa October 21
  • Stand United 3 – 0 Maji Maji FC 
  • Coastal Union 1 – 0 Kagera Sugar
DSC_0077
Tambwe akiwania mpira na Hamisi Kasanga
DSC_0069
Juma Abdul akijaribu kumtoka Robert Magadula
DSC_0078
Haruna Niyonzima akipiga krosi
DSC_0050
Simon Msuva akijaribu kumtoka beki wa Toto
DSC_0054
Donald Ngoma akijaribu kupiga krosi iliyozuiliwa na Hamis Kasanga
DSC_0057
Niyonzima na Juma Abdul wakishangilia goli lao la kwanza
ya
Simon Msuva akishangilia na Coutinho baada ya kufunga goli
yang
Amissi Tambwe akishangilia goli na Simon Msuva

0 comments: