Serikali ya Japan imesema iko
tayari kutoa dawa waliotengeneza ya kupambana na homa kali iitwayo T-705
ambayo huenda ikasaidia katika vita vya kupambana na Homa ya EBOLA.
Matumizi ya dawa hiyo hayajaidhinishwa na
shirika la afya duniani World Health Organisation, haijabainika iwapo
itafaa kutoa afueni kwa wagonjwa wa Ebola au la .Akiongeza alisema kwamba Kampuni hiyo ya Fujifilm inafanya mazungumzo na utawala wa chakula na dawa Marekani juu ya kupimwa uwezo wa dawa hiyo kuhusiana na matibabu ya Ebola.
Kwa sasa hamna dawa wala chanjo yoyote iliyothibitika na kuidhinishwa kutibu Ebola, lakini kutokana na janga la mlipuko wa Ebola huko Afrika magharibi na sasa Jamhuri ya Kidemocrasi ya Congo, Shirika la afya duniani WHO limesema itakubali matumzi ya dawa za majaribio kwa wagonjwa, ilimradi utaratibu na masharti waliyoyaweka yafuatwe na wagonjwa wenyewe wahusishwe katika kutoa idhini .
Majuzi wamarekani wawili waliokuwa wamethibishwa kuugua Ebola walipona baada ya kupewa dawa ya majaribio iitwayo ZMapp.
Aliongezea kusema kwamba Japan inangoja maelezo zaidi ya uamuzi wa WHO kuhusu matumizi ya dawa ambazo hazijajaribiwa lakini katika kesi yoyote ya dharura, Japan inaweza ikajibu maagizo yoyote ya kibinafsi hata kabla ya uamuzi wowote wa WHO.
Mapema mwezi huu WHO ilisema kwamba ni sawa kutumia dawa ambazo hazijajaribiwa kwa wagonjwa wa Ebola kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo.
0 comments:
Post a Comment