Makamu
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu akiwaeleza
jambo Wawakilishi wa Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) kuhusu mapendekezo
yao waliyoyawasilisha kwake kwaajili ya Katiba Mpya jana 26 Agosti,
2014.
Chifu
John Nyanza (aliyekaa katikati) wa kutoka Magu akimueleza jambo Makamu
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu (kulia) juu ya
uwasilishaji wa mapendekezo yao kwa ajili ya Katiba Mpya alipokutana
naye jana 26 Agosti, 2014. kwenye Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge
Maalum.
Chifu
Agnes Ndaturu (kushoto) wa kutoka Ntuzu, Bariadi akimueleza jambo
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu (kulia)
juu ya uwasilishaji wa mapendekezo yao kwa ajili ya Katiba Mpya
alipokutana naye jana 26 Agosti, 2014. kwenye Ofisi ya Makamu Mwenyekiti
wa Bunge Maalum.
Makamu
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu (kulia)
akipokea mapendekezo ya maoni toka kwa Chifu John Nyanza alieuwakilisha
Umoja wa Machifu wa Tanzania (UMT) jana 26 Agosti, 2014.kwenye Ofisi ya
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari walikifuatilia uwasilishwaji wa mapendekezo toka
kwa Machifu waliouwakilisha Umoja wa Machifu wa Tanzania (UMT) jana 26
Agosti, 2014.kwenye Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
(Picha zote na Benedict Liwenga-Maelezo, Dodoma)
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
UMOJA wa Machifu wa Tanzania (UMT)
kupitia wawakilishi wake, jana 26 Agosti, 2014 umewasilisha nyongeza ya
mapendekezo yake kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya kwa Makamu Mwenyekiti wa
Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Akiuwakilisha Umoja wa Machifu
Tanzani (UMT), Chifu kutoka Magu John Nyanza amemueleza Makamu
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba kuwa wanaishauri Serikali
kutayarisha mkakati wa Kitaifa wa Utamaduni kwa kuwashirikisha wadau
wakuu wa masuala ya Utamaduni ili mpango mkakati huo uwe na Dira ya
Utamaduni itakayobainisha cha kufanya ili kujenga, kuhamasisha na
kuendeleza Utamduni katika maeneo yote nchini.
“Chifu kutoka Magu, John Nyanza
amesema kuwa lengo la kuwasilisha mapendekezo hayo kwaajili ya
kusisitiza masuala mazuri ya Utamduni kuendelea ili kuweza kudumisha
madili kwa nia nzuri ya kudumisha amni na ushirikiano”. Alisema Chifu
Nyanza.
Naye Chifu kutoka Ntuzu, Bariadi
Chifu Agnes Ndaturu ameeleza kuwa mapendekezo yao yatasaidia kuweza
kuwatambua waganga wa Jadi ambapo hapo zamani , mganga wa Jadi alikuwa
anatambulika na kufanya kazi katika eneo husika analotoka, lakini hivi
sasa waganga wengi wa jadi wamekuwa na tabia ya kufanya kazi zao bila
mipaka.
”Mapendekezo haya yatasaidia
viongozi wa waganga wa jadi nchini kuwatambua wale waganga wanaokiuka
maadili ya shughuli zao mfano mauaji ya Albino, kwakuwa kila kiongozi
atakuwa anawatambua waganga wa eneo lake husika”. Alisema Chifu Ndaturu.
Aidha, Machifu hao wameongeza
kuwa, Wajumbe wenzao waliowatuma kuwawakilisha wanasisitiza juu ya
umuhimu wa Utamaduni kupewa nafasi rasmi katika Katiba mpya na Serikali
ili pawepo na kipaumbele katika utekelezaji wake nchini.
Wakizungumza kwa kauli moja Umoja
wa Machifu wa Tanzania wamesema kuwa suala la Utamaduni katika Rasimu ya
Pili ya Katiba lifanyiwe marekebisho kwa kuzingatia mapendekezo
yaliyoibainishwa huku msisitizo wao ukiwa katika Katiba kueleza wazi
kuwa sera na Sheria mpya zitakazotungwa zihakikishe kuwa Tume ya Taifa
ya Utamaduni inaanzishwa kisheria ili kusimamia masuala ya Utamaduni.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Bunge
Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewatotoa wasiwasi
wawakilishi wa Umoja wa Machifu hao wa Tanzania aliokutana nao kwa
kuwaeleza kuwa atayawasilisha katika Uongozi wa Kamati ya Bunge ambapo
Kamati Ndogo ya Uongozi inatarajiwa kukutana leo jioni ili kuweza
kuyajadili.
“Nimeyapokea mapendekezo yenu,
kwakuwa Kamati zinaendelea na kazi ambapo wiki hii kamati zitakuwa
zimemaliza kazi zake na hakutakuwa na nafasi tena ya kuyapokea
mapendekezo na maoni mengine”. Alisema Samia.
Hivi karibuni, makundi mbalimbali
yaliwasilisha mapendekezo yao ambapo baadhi ya makundi hayo yakiwemo
Wafugaji, Wasanii na Wanahabari yaliwasilisha.
Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
26/08/2014.
0 comments:
Post a Comment