Saturday, 23 August 2014

SNURA APELEKA ‘MAJANGA’ TARIME MKOANI MARA



NA MWANDISHI WETU
MWANAMUZIKI mahiri Tanzania na Afrika Mashariki katika mtindo wa mduara, Snura Mushi, anatarajiwa kutumbuiza kwenye Viwanja Vya Nyamongo, Rorya, onyesho ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake.

Akizungumza kutoka Tarime, Mkurugenzi wa Taasisi ya Nyumbani Kwanza Media Group, Mossy Magere alisema msanii huyo atafanya onyesho baada ya maandamano ya Jumapili ya kupinga ukatili wa kijinsia.

Snura aliyvuma zaidi na kibao chake cha Majanga anatarajiwa kuwasili Rorya leo kwa ajili ya onyesho hilo.
Magere alisema lengo la maandamano hayo yatakayoongozwa na RPC wa Tarime-Rorya, Lazaro Mambosasa ni kuhamasisha jamii kuachana na ukatili dhidi ya wanawake.

Maandamano hayo yataanza saa 3:30 katika Hospitali ya Nyamongo na kuishia Shule ya Msinga Nyamongo.

0 comments: